1 Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaushambulia mji wa Gaza:
2 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Tazama! Maji yanapanda kutoka kaskazini,nayo yatakuwa mto uliofurika;yataifunika nchi nzima na vyote vilivyomo,mji na wakazi na wanaoishi humo.Watu watalia,wakazi wote wa nchi wataomboleza.
3 Watasikia mshindo wa kwato za farasi,kelele za magari ya vita,na vishindo vya magurudumu yao.Kina baba watawasahau watoto wao,mikono yao itakuwa imelegea mno.
4 Hiyo ni siku ya kuwaangamiza Wafilisti wote,kukomesha msaada uliobakia kutoka Tiro na Sidoni.Maana Mwenyezi-Mungu anawaangamiza Wafilisti,watu waliosalia wa kisiwa cha Kaftori.
5 Watu wa Gaza wamenyoa upara kuomboleza;mji wa Ashkeloni umeangamia.Enyi watu wa Anakimu mliobakimpaka lini mtajikatakata kwa huzuni?
6 Ee upanga wa Mwenyezi-Mungu!Utachukua muda gani ndipo utulie?Ingia katika ala yako,ukatulie na kunyamaa!
7 Lakini utawezaje kutulia,hali Mwenyezi-Mungu ameupa kazi?Ameuamuru ushambulie mji wa Ashkelonina watu wanaoishi pwani.”