10 kisha taifa hilo likafanya uovu mbele yangu na kukataa kunitii, basi, mimi nitaacha kulitendea mema hayo niliyokusudia kulitendea.
11 Sasa, basi, waambie watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mimi Hufinyanga jambo ovu dhidi yenu na kufanya mpango dhidi yenu. Rudini na kuacha njia zenu mbaya, mkarekebishe mienendo yenu na matendo yenu.
12 Lakini wao watasema, ‘Hiyo ni bure tu! Tutafuata mipango yetu wenyewe na kila mmoja wetu atafanya kwa kiburi kadiri ya moyo wake mwovu.’”
13 Basi, Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Yaulize mataifa yote:Nani amewahi kusikia jambo kama hili.Israeli amefanya jambo la kuchukiza mno.
14 Je, majabali ya Lebanoni hukosa theluji?Je, vijito vya maji vya milima yake hukauka?
15 Lakini watu wangu wamenisahau mimi,wanafukizia ubani miungu ya uongo.Wamejikwaa katika njia zao,katika barabara za zamani.Wanapitia vichochoroni badala ya njia kuu.
16 Wameifanya nchi yao kuwa kitisho,kitu cha kuzomewa daima.Kila mtu apitaye huko hushangaana kutikisa kichwa chake.