4 Kwa maana watu wameniacha mimi na kupatia unajisi mahali hapa kwa kufukizia ubani miungu mingine; miungu ambayo wao wenyewe, wazee wao wala wafalme wa Yuda hawajapata kuijua. Pia wamepajaza mahali hapa damu ya watu wasio na hatia,
5 wakamjengea mungu Baali madhabahu, ili kuwachoma wana wao kama sadaka ya kuteketezwa. Mimi sijapata kuamuru wala kuagiza jambo kama hilo lifanywe, wala hata sijapata kulifikiria.
6 Kwa hiyo, jueni kuwa siku zaja ambapo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala bonde la Mwana wa Hinomu, bali pataitwa bonde la Mauaji. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
7 Na papa hapa nitaivuruga mipango ya Yuda na Yerusalemu. Nitawafanya watu wao washindwe na kuuawa na maadui zao vitani na kuangamizwa na wale wanaowawinda. Maiti zao nitawaachia ndege wa anga na wanyama wa porini kuwa chakula chao.
8 Nitaufanya mji huu kuwa mahali pa kushangaza; naam, nitaufanya uwe kitu cha kuzomewa. Kila mtu anayepita karibu nao atashangaa na kuuzomea kwa sababu ya maafa yote yatakayoupata.
9 Maadui watauzingira na kujaribu kuwaua watu wake. Watasababisha hali mbaya sana mjini humo hata watu watawala watoto wao wa kike na wa kiume, na kila mtu atamla mwenzake.
10 Kisha wewe utalivunja gudulia hilo mbele ya watu hao watakaokwenda pamoja nawe,