33 Kweli wewe ni bingwa wa kutafuta wapenzi!Hata wanawake wabaya huwafundisha njia zako.
34 Nguo zako zina damu ya maskini wasio na hatia,japo hukuwakuta wakivunja nyumba yako.“Lakini licha ya hayo yote,
35 wewe wasema: ‘Mimi sina hatia;hakika hasira yake imegeuka mbali nami.’Lakini mimi nitakuhukumu kwa sababu unasema:‘Sikutenda dhambi.’
36 Kwa nini unajirahisisha hivi,ukibadilibadili mwenendo wako?Utaaibishwa na Misri,kama ulivyoaibishwa na Ashuru.
37 Na huko pia utatoka,mikono kichwani kwa aibu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimewakataa wale uliowategemea,wala hutafanikiwa kwa msaada wao.