19 Sikiliza kilio cha watu wangu,kutoka kila upande katika nchi.“Je, Mwenyezi-Mungu hayuko Siyoni?Je, mfalme wake hayuko tena huko?”“Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao za miungu,na vinyago vyao vya miungu ya kigeni?”
20 “Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha,nasi bado hatujaokolewa!
21 Jeraha la watu wangu limeniumiza moyoni,ninaomboleza na kufadhaika.
22 Je, hakuna dawa ya kupaka huko Gileadi?Je, hakuna mganga huko?Mbona basi watu wangu hawajaponywa?