5 Lisikilizeni neno la BWANA, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe BWANA, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.
6 Sauti ya fujo itokayo mjini!Sauti itokayo hekaluni!Sauti ya BWANA awalipaye adui zake adhabu!
7 Kabla hajaona utungu alizaa;Kabla maumivu yake hayajampata,Alizaa mtoto mwanamume.
8 Ni nani aliyesikia neno kama hili?Ni nani aliyeona mambo kama haya?Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja?Taifa laweza kuzaliwa mara?Maana Sayuni, mara alipoona utungu,Alizaa watoto wake.
9 Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.
10 Furahini pamoja na Yerusalemu, shangilieni kwa ajili yake, ninyi nyote mmpendao; furahini pamoja naye kwa furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake;
11 mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake.