2 Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Wewe mtu, hawa ndio watu watungao uovu na kutoa mashauri mabaya mjini humu.
3 Wanasema, ‘Wakati wa kujenga nyumba bado. Mji ni kama chungu, na sisi ni kama nyama.’
4 Kwa hiyo, toa unabii dhidi yao! Tabiri ewe mtu!”
5 Kisha roho ya Mwenyezi-Mungu ikanijia, naye akaniambia, “Waambie watu, Mwenyezi-Mungu asema hivi: Naam, hiki ndicho mnachofikiri enyi Waisraeli. Najua mambo mnayofikiria moyoni mwenu.
6 Nyinyi mmewaua watu wengi mjini humu, na kujaza barabara zake na watu waliouawa.
7 “Lakini, mimi, Bwana Mwenyezi-Mungu nasema: Naam, mji huu ni chungu cha kupikia, na wale waliouawa ndio nyama. Nyinyi lazima mtaondolewa mjini.
8 Nyinyi mmeogopa upanga? Basi, mimi nitaleta upanga dhidi yenu!