9 Sasa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nakuuliza:Je, mzabibu huo utaweza kustawi?Je, hawatangoa mizizi yakena kuozesha matunda yakena matawi yake machanga kuyanyausha?Hakutahitajika mtu mwenye nguvu au jeshikuungoa kutoka humo ardhini.
10 Umepandikizwa, lakini, je, utastawi?Upepo wa mashariki uvumapo juu yake utanyauka;utanyauka papo hapo kwenye kuta ulikoota.”
11 Kisha neno la Mwenyezi-Mungu likanijia:
12 “Sasa waulize hao watu waasi kama wanaelewa maana ya mfano huo. Waambie kuwa, mfalme wa Babuloni alikuja Yerusalemu, akamwondoa mfalme na viongozi wake, akawapeleka Babuloni.
13 Kisha akamtawaza mmoja wa jamaa ya kifalme, akafanya naye mapatano, akamwapisha. Aliwaondoa humo nchini watu mashujaa akawapeleka mbali
14 ili utawala huo uwe dhaifu na uzingatie agano lake mfalme wa Babuloni.
15 Lakini yule mfalme mpya alimwasi mfalme wa Babuloni kwa kuwatuma wajumbe Misri kuomba farasi na askari wengi. Je, mfalme huyo atafaulu? Je, anayefanya hivyo na kuvunja agano lake ataweza kuepa adhabu?