19 Vedani na Yavani walisafirisha bidhaa zako toka Uzali; hata chuma kilichofuliwa, mdalasini na mchaichai ili kupata bidhaa zako.
20 Watu wa Dedani walifanya biashara nawe kwa kukupatia matandiko ya farasi.
21 Waarabu na wakuu wote wa nchi ya Kedari walikuwa wachuuzi wako wakuu katika biashara ya wanakondoo, kondoo madume na mbuzi.
22 Wachuuzi wa Sheba na wa Rama walifanya biashara nawe; walikuletea viungo vya chakula, vito vya thamani na dhahabu kujipatia bidhaa zako safi.
23 Wakazi wa miji ya Harani, Kane na Edeni na wachuuzi wa Ashuru na Kilmadi walifanya biashara nawe.
24 Hao walifanya nawe biashara ya mavazi ya fahari, nguo za buluu zilizotariziwa, mazulia ya rangi angavu vifundo na kamba zilizosokotwa imara.
25 Merikebu za Tarshishi ndizo zilikusafirishia bidhaa zako.Basi kama meli katikati ya bahariwewe ulikuwa umejaa shehena.