10 Balaki akawaka hasira dhidi ya Balaamu, akakunja mikono kwa ghadhabu na kumwambia, “Nilikuita uwalaani adui zangu, lakini mara hizi zote tatu umewabariki!
11 Sasa! Nenda zako. Nilikuwa nimekuahidi kukupa zawadi nyingi, lakini Mwenyezi-Mungu hakukujalia kupata zawadi hizo, amekunyima!”
12 Balaamu akamjibu Balaki, “Je, sikuwaambia wajumbe uliowatuma kwangu
13 kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kukiuka agizo la Mwenyezi-Mungu, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa hiari yangu mwenyewe? Nilisema, atakachosema Mwenyezi-Mungu ndicho nitakachokisema.
14 “Sasa ninarudi kwa watu wangu, lakini kabla sijaondoka, acha nikuambie mambo ambayo watu hao watawatendea watu wako siku zijazo.”
15 Basi, Balaamu akatamka kauli hii:“Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Beori,kauli ya mtu aliyefumbuliwa macho,
16 kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu,na mtu ajuaye maarifa ya Mungu Mkuu,mtu aonaye maono ya Mungu Mwenye Nguvu,mtu anayesujudu, macho wazi.