3 Lilimjia tena wakati Yehoyakimu mwana wa Yosia, alipokuwa mfalme wa Yuda. Yeremia aliendelea kupata neno la Mwenyezi-Mungu hadi mwishoni mwa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Mnamo mwezi wa tano wa mwaka huo, watu wa Yerusalemu walipelekwa uhamishoni.
4 Mwenyezi-Mungu aliniambia neno lake:
5 “Kabla hujachukuliwa mimba, mimi nilikujua,kabla hujazaliwa, mimi nilikuweka wakfu;nilikuteua uwe nabii kwa mataifa.”
6 Nami nikajibu, Aa! Bwana Mwenyezi-Mungu,mimi sijui kusema, kwa kuwa bado ningali kijana.
7 Lakini Mwenyezi-Mungu akaniambia,“Usiseme kwamba wewe ni kijana bado.Utakwenda kwa watu wote nitakaokutuma kwao,na yote nitakayokuamuru utayasema.
8 Wewe usiwaogope watu hao,kwa maana niko pamoja nawe kukulinda.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
9 Kisha Mwenyezi-Mungu akaunyosha mkono wake, akagusa kinywa changu, akaniambia,“Tazama nimeyatia maneno yangu kinywani mwako.