4 Mwenyezi-Mungu aliniambia neno lake:
5 “Kabla hujachukuliwa mimba, mimi nilikujua,kabla hujazaliwa, mimi nilikuweka wakfu;nilikuteua uwe nabii kwa mataifa.”
6 Nami nikajibu, Aa! Bwana Mwenyezi-Mungu,mimi sijui kusema, kwa kuwa bado ningali kijana.
7 Lakini Mwenyezi-Mungu akaniambia,“Usiseme kwamba wewe ni kijana bado.Utakwenda kwa watu wote nitakaokutuma kwao,na yote nitakayokuamuru utayasema.
8 Wewe usiwaogope watu hao,kwa maana niko pamoja nawe kukulinda.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
9 Kisha Mwenyezi-Mungu akaunyosha mkono wake, akagusa kinywa changu, akaniambia,“Tazama nimeyatia maneno yangu kinywani mwako.
10 Leo nimekupa mamlaka juu ya mataifa na falme,uwe na mamlaka ya kungoa na kubomoa,mamlaka ya kuharibu na kuangamiza,mamlaka ya kujenga na ya kupanda.”