1 Sikilizeni neno analowaambieni Mwenyezi-Mungu,enyi Waisraeli!
2 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Msijifunze mienendo ya mataifa mengine,wala msishangazwe na ishara za mbinguni;yaacheni mataifa mengine yashangazwe nazo.
3 Maana, mila za dini za watu hawa ni za uongo.Mtu hukata mti msitunifundi akachonga kinyago cha mungu kwa shoka.
4 Kisha watu hukipamba kwa fedha na dhahabuwakakipigilia misumari kwa nyundoili kisije kikaanguka.
5 Vinyago vyao ni kama vinyago vya kutishia ndegekatika shamba la matango,havina uwezo wa kuongea;ni lazima vibebwemaana haviwezi kutembea.Msiviogope vinyago hivyo,maana haviwezi kudhuru,wala haviwezi kutenda lolote jema.”
6 Ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe;wewe ni mkuu na nguvu yako yajulikana.