12 Mwenyezi-Mungu aliiumba dunia kwa nguvu zake;kwa hekima yake aliuimarisha ulimwengu,kwa akili yake alizitandaza mbingu.
13 Anapotoa sauti yake, maji hunguruma mbinguni,huzusha ukungu kutoka mipaka ya dunia.Huufanya umeme umulike wakati wa mvua,na kuutoa upepo katika ghala zake.
14 Binadamu ni mjinga na mpumbavu;kila mfua dhahabu huaibishwa na vinyago vyake;maana, vinyago hivyo ni uongo mtupu.Havina uhai wowote ndani yao.
15 Havina thamani, ni udanganyifu mtupu;wakati vitakapoadhibiwa vyote vitaangamia.
16 Lakini Mungu wa Yakobo si kama vinyago hivyo,maana, yeye ndiye aliyeumba vitu vyote,na Israeli ni taifa lililo mali yake;Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.
17 Kusanyeni vitu vyenu enyi watu mliozingirwa.
18 Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Wakati huo nitawatupa nje ya nchi hii,nitawataabisha asibaki mtu yeyote.”