18 Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Wakati huo nitawatupa nje ya nchi hii,nitawataabisha asibaki mtu yeyote.”
19 Ole wangu mimi Yerusalemu maana nimejeruhiwa!Jeraha langu ni baya sana!Lakini nilisema: “Hakika haya ni mateso,na sina budi kuyavumilia.”
20 Lakini hema langu limebomolewa,kamba zake zote zimekatika;watoto wangu wameniacha, na kwenda zao,wala hawapo tena;hakuna wa kunisimikia tena hema langu,wala wa kunitundikia mapazia yangu.
21 Nami Yeremia nikasema:Wachungaji wamekuwa wajinga,hawakuomba shauri kwa Mwenyezi-Mungu;kwa sababu hiyo, hawakufanikiwa,na kondoo wao wote wametawanyika.
22 Sikilizeni sauti! Habari zinatufikia.Kuna kishindo kutoka kaskazini.Taifa kutoka kaskazini linakuja,kuifanya miji ya Yuda kuwa jangwaambamo kutakuwa na mapango ya mbweha!
23 Najua, ee Mwenyezi-Mungu,binadamu hana uwezo na maisha yake;hakuna mtu awezaye kuyaongoza maisha yake.
24 Utukosoe, ee Mwenyezi-Mungu, lakini si kwa ghadhabu,wala kwa hasira yako, tusije tukaangamia.