9 Vinyago hivyo hupambwa kwa fedha kutoka Tarshishi,na dhahabu kutoka Ofiri;kazi ya mafundi stadi na wafua dhahabu.Zimevishwa nguo za samawati na zambarau,zilizofumwa na wafumaji stadi.
10 Lakini Mwenyezi-Mungu ni Mungu wa kweli;Mungu aliye hai, mfalme wa milele.Akikasirika, dunia hutetemeka,mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.
11 Basi, utawaambia hivi: “Miungu ambayo haikuumba mbingu na dunia, itaangamia. Itatoweka kabisa duniani na chini ya mbingu.”
12 Mwenyezi-Mungu aliiumba dunia kwa nguvu zake;kwa hekima yake aliuimarisha ulimwengu,kwa akili yake alizitandaza mbingu.
13 Anapotoa sauti yake, maji hunguruma mbinguni,huzusha ukungu kutoka mipaka ya dunia.Huufanya umeme umulike wakati wa mvua,na kuutoa upepo katika ghala zake.
14 Binadamu ni mjinga na mpumbavu;kila mfua dhahabu huaibishwa na vinyago vyake;maana, vinyago hivyo ni uongo mtupu.Havina uhai wowote ndani yao.
15 Havina thamani, ni udanganyifu mtupu;wakati vitakapoadhibiwa vyote vitaangamia.