17 Nitawatawanya mbele ya adui,kama upepo utokao mashariki.Nitawapa kisogo badala ya kuwaonesha uso wangusiku hiyo ya kupata maafa yao.”
18 Kisha, watu wakasema: “Njoni tumfanyie Yeremia njama, maana hatukosi makuhani wa kutufundisha, wenye hekima wa kutushauri na manabii wa kututangazia ujumbe wa Mungu! Njoni tumshtaki kwa maneno yake mwenyewe, wala tusiyatilie maanani yote asemayo.”
19 Basi, mimi nikasali:Nitegee sikio ee Mwenyezi-Mungu,usikilize ombi langu.
20 Je, mtu hulipwa mabaya kwa mema?Walakini, wamenichimbia shimo.Kumbuka nilivyosimama mbele yako,nikasema mema kwa ajili yao,ili kuiepusha hasira yako mbali nao.
21 Kwa hiyo waache watoto wao wafe njaa,waache wafe vitani kwa upanga.Wake zao wawe tasa na wajane.Waume zao wafe kwa maradhi mabayana vijana wao wachinjwe kwa upanga vitani.
22 Kilio na kisikike majumbani mwao,unapowaletea kundi la wanyanganyi ghafla.Maana wamechimba shimo waninase;wameitegea mitego miguu yangu.
23 Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu,wazijua njama zao zote za kuniua.Usiwasamehe uovu wao,wala kufuta dhambi zao.Waanguke chini mbele yako;uwakabili wakati wa hasira yako.