27 Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nchi nzima itakuwa jangwa tupu;lakini sitaiharibu kabisa.
28 Kwa hiyo, nchi itaomboleza,na mbingu zitakuwa nyeusi.Maana, nimetamka na sitabadili nia yangu;nimeamua, wala sitarudi nyuma.
29 Watakaposikika wapandafarasi na wapiga mishale,kila mmoja atatimua mbio.Baadhi yao watakimbilia msituni,wengine watapanda majabali.Kila mji utaachwa tupu;hakuna mtu atakayekaa ndani.
30 Nawe Yerusalemu uliyeachwa tupu,unavalia nini mavazi mekundu?Ya nini kujipamba kwa dhahabu,na kujipaka wanja machoni?Unajirembesha bure!Wapenzi wako wanakudharau sana;wanachotafuta ni kukuua.
31 Nilisikia sauti kama ya mwanamke anayejifungua,yowe kama anayejifungua mtoto wa kwanza.Ilikuwa sauti ya Yerusalemu akitweta,na kuinyosha mikono yake akisema,‘Ole wangu!Wanakuja kuniua!’”