1 Haya ndiyo maneno aliyotamka nabii Yeremia mnamo mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia naye Baruku mwana wa Neria akawa anayaandika kitabuni.Yeremia alimwambia Baruku:
2 “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi juu yako wewe Baruku:
3 Wewe ulisema, ‘Ole wangu! Mwenyezi-Mungu ameniongezea uchungu juu ya maumivu yangu. Nimechoka kupiga kite, wala sipati pumziko.’
4 Lakini Mwenyezi-Mungu ameniambia nikuambie hivi: Tazama, yale niliyojenga nayabomoa, na yale niliyopanda nayangoa; nitafanya hivyo katika nchi yote.