10 Siku hiyo ni siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi,ni siku ya kulipiza kisasi;naam, siku ya kuwaadhibu maadui zake.Upanga utawamaliza hao na kutosheka,utainywa damu yao na kushiba.Maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anayo kafarahuko kaskazini karibu na mto Eufrate.