7 Nani huyo aliye kama mto Nili uliofurikakama mito inayoumuka mawimbi?
8 Misri ni kama mto Nili uliofurikakama mito inayoumuka mawimbiIlisema: “Nitajaa, nitaifunika nchi,nitaiharibu miji na wakazi wake.
9 Songeni mbele, enyi farasi,shambulieni enyi magari ya farasi.Mashujaa wasonge mbele:Watu wa Kushi na Puti washikao ngao,watu wa Ludi, stadi wa kutumia pinde.”
10 Siku hiyo ni siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi,ni siku ya kulipiza kisasi;naam, siku ya kuwaadhibu maadui zake.Upanga utawamaliza hao na kutosheka,utainywa damu yao na kushiba.Maana Mwenyezi-Mungu wa majeshi anayo kafarahuko kaskazini karibu na mto Eufrate.
11 Pandeni Gileadi, enyi watu wa Misri,mkachukue dawa ya marhamu.Mmetumia dawa nyingi bure;hakuna kitakachowaponya nyinyi.
12 Mataifa yamesikia aibu yenu,kilio chenu kimeenea duniani kote;mashujaa wamegongana wenyewe kwa wenyewe,wote pamoja wameanguka.
13 Neno ambalo Mwenyezi-Mungu alimwambia Yeremia wakati alipofika Nebukadneza mfalme wa Babuloni kuishambulia nchi ya Misri: