23 Wataukata kabisa msitu wake, ingawa haupenyeki,nasema mimi Mwenyezi-Mungu,maana wao ni wengi kuliko nzige wasiohesabika.
24 Watu wa Misri wataaibishwa,watatiwa mikononi mwa watu kutoka kaskazini.”
25 Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, alisema: “Tazama, mimi nitamwadhibu Amoni mungu wa Thebesi, nitaiadhibu Misri na miungu yake na wafalme wake, nitamwadhibu Farao na wote wanaomtegemea.
26 Nitawatia mikononi mwa wale wanaotaka kuyaangamiza maisha yao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babuloni na maofisa wake. Baadaye, nchi ya Misri itakaliwa na watu kama ilivyokuwa hapo zamani. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
27 “Lakini wewe usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,usifadhaike, ee Israeli;maana, kutoka mbali nitakuokoa,nitakuja kuwaokoa wazawa wakokutoka nchi walimohamishwa.Yakobo utarudi na kutulia na kustarehe,wala hakuna yeyote atakayekutia hofu.
28 Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,kwa maana mimi niko pamoja nawe.Nitayaangamiza kabisa mataifa yoteambayo nimekutawanya kati yao,lakini wewe sitakuangamiza.Nitakuchapa kadiri unavyostahili,sitakuacha bila kukuadhibu.”