1 Enyi watu wa Benyamini,ondokeni Yerusalemu mkimbilie usalama!Pigeni tarumbeta mjini Tekoa;onesheni ishara huko Beth-hakeremu,maana maafa na maangamizi makubwayanakuja kutoka upande wa kaskazini.
2 Mji wa Siyoni ni mzuri na mwororo,lakini utaangamizwa.
3 Watu wataujia kama wachungaji na makundi yao,watapiga hema zao kuuzunguka kila mmoja sehemu yake,wapate kuyaongoza makundi yao.
4 Watasema: “Jitayarisheni kuushambulia Siyoni.Haya! Tuanze kushambulia adhuhuri!Bahati mbaya; jua linatua!Kivuli cha jioni kinarefuka.
5 Basi, tutaushambulia usiku;tutayaharibu majumba yake ya kifalme.”
6 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema:“Kateni miti yake,rundikeni udongo kuuzingira Yerusalemu.Mji huu ni lazima uadhibiwe,maana hamna lolote ndani yake ila dhuluma.