4 Watasema: “Jitayarisheni kuushambulia Siyoni.Haya! Tuanze kushambulia adhuhuri!Bahati mbaya; jua linatua!Kivuli cha jioni kinarefuka.
5 Basi, tutaushambulia usiku;tutayaharibu majumba yake ya kifalme.”
6 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema:“Kateni miti yake,rundikeni udongo kuuzingira Yerusalemu.Mji huu ni lazima uadhibiwe,maana hamna lolote ndani yake ila dhuluma.
7 Kama kisima kinavyohifadhi maji yake yakabaki safi,ndivyo Yerusalemu unavyohifadhi uovu wako.Ukatili na uharibifu vyasikika ndani yake,magonjwa na majeraha yake nayaona daima.
8 Hilo na liwe onyo kwako ee Yerusalemu,la sivyo nitakutupa kabisa kwa chuki;nikakufanya uwe jangwa,mahali pasipokaliwa na mtu.”
9 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:“Kusanyeni watu wote wa Israeli waliobakikama watu wakusanyavyo zabibu zote;kama afanyavyo mchumazabibu,pitisheni tena mikono yenu katika matawi yake.”
10 Nitaongea na nani nipate kumwonya,ili wapate kunisikia?Tazama, masikio yao yameziba,hawawezi kusikia ujumbe wako.Kwao neno lako, ee Mwenyezi-Mungu,limekuwa jambo la dhihaka,hawalifurahii hata kidogo.