7 Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa;alikuwa na mabawa makubwa ya manyoya mengi.Basi, ule mzabibu ukamtandia mizizi yake,ukamwelekezea matawi yake,ili aumwagilie maji.
8 Mzabibu ulikuwa umetolewa kitaluni mwakeukapandikizwa penye udongo mzuri na maji mengi,ili upate kutoa matawi na kuzaa matundauweze kuwa mzabibu mzuri sana!
9 Sasa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nakuuliza:Je, mzabibu huo utaweza kustawi?Je, hawatangoa mizizi yakena kuozesha matunda yakena matawi yake machanga kuyanyausha?Hakutahitajika mtu mwenye nguvu au jeshikuungoa kutoka humo ardhini.
10 Umepandikizwa, lakini, je, utastawi?Upepo wa mashariki uvumapo juu yake utanyauka;utanyauka papo hapo kwenye kuta ulikoota.”
11 Kisha neno la Mwenyezi-Mungu likanijia:
12 “Sasa waulize hao watu waasi kama wanaelewa maana ya mfano huo. Waambie kuwa, mfalme wa Babuloni alikuja Yerusalemu, akamwondoa mfalme na viongozi wake, akawapeleka Babuloni.
13 Kisha akamtawaza mmoja wa jamaa ya kifalme, akafanya naye mapatano, akamwapisha. Aliwaondoa humo nchini watu mashujaa akawapeleka mbali