17 Lakini macho yako wewe na moyo wako,hungangania tu mapato yasiyo halali.Unamwaga damu ya wasio na hatia,na kuwatendea watu dhuluma na ukatili.
18 “Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi juu ya Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda:Wakati atakapokufa,hakuna atakayemwombolezea akisema,‘Ole, kaka yangu!’‘Ole, dada yangu!’Hakuna atakayemlilia akisema,‘Maskini, bwana wangu!’‘Maskini, mfalme wangu!’
19 Atazikwa bila heshima kama punda,ataburutwa na kutupiliwa mbali,nje ya malango ya Yerusalemu.”
20 Enyi watu wa Yerusalemu,pandeni Lebanoni mpige kelele,pazeni sauti zenu huko Bashani;lieni kutoka milima ya Abarimu,maana wapenzi wenu wote wameangamizwa.
21 Mwenyezi-Mungu aliongea nanyi mlipokuwa na fanaka,lakini nyinyi mkasema, “Hatutasikiliza.”Hii ndiyo tabia yenu tangu ujana wenu,hamjapata kuitii sauti ya Mwenyezi-Mungu.
22 Viongozi wenu watapeperushwa na upepo,wapenzi wenu watachukuliwa uhamishoni.Ndipo mtakapoona haya na kufadhaika,kwa sababu ya uovu wenu wote mliotenda.
23 Enyi wakazi wote wa Lebanoni,nyinyi mkaao salama kati ya mierezi;jinsi gani mtakavyopiga kite uchungu utakapowakumba,uchungu kama wa mama anayejifungua!