26 Nitakufukuzia mbali katika nchi ya kigeni, wewe pamoja na mama yako mzazi. Mtakuwa watumwa katika nchi hiyo ambamo nyote wawili hamkuzaliwa, nanyi mtafia hukohuko.
27 Mtatamani kwa hamu kubwa kurudi katika nchi hii, lakini hamtarudi kamwe.
28 Je, huyu mtu Konia,amekuwa kama chungu kilichovunjika,ambacho hudharauliwa na kutupwa nje?Kwa nini yeye na watoto wake wametupwa mbaliwakatupwa katika nchi wasiyoijua?
29 Ee nchi, ee nchi, ee nchi!Sikia neno la Mwenyezi-Mungu!
30 Mwenyezi-Mungu asema hivi:Mwandike mtu huyu kwamba hana watoto,mtu ambaye hatafanikiwa maishani mwake.Maana hakuna hata mmoja wa wazawa wakeatakayekikalia kiti cha enzi cha Daudina kutawala tena katika Yuda.