24 Mwenyezi-Mungu aliniagiza nimwambie hivi Shemaya wa Nehelamu:
25 “Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Umepeleka barua kwa jina lako kwa wakazi wote wa Yerusalemu na kwa kuhani Sefania mwana wa Maaseya na kwa makuhani wengine wote. Katika barua hiyo, ulimwambia Sefania hivi:
26 ‘Mwenyezi-Mungu amekufanya wewe Sefania kuwa kuhani badala ya kuhani Yehoyada, uwe mkuu wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Ni wajibu wako kumtia gerezani na kumfunga minyororo mwendawazimu yeyote anayetabiri.
27 Kwa nini basi, hukumkemea Yeremia kutoka Anathothi anayekutabiria?
28 Maana yeye alituma taarifa huko Babuloni kwamba uhamisho wenu utakuwa wa muda mrefu, na kusema mjenge nyumba, mkae; mlime mashamba, mpande mbegu na kula mazao yake!’”
29 Kuhani Sefania aliisoma barua hiyo mbele ya nabii Yeremia.
30 Ndipo Mwenyezi-Mungu akamwambia Yeremia: