27 Yeremia, wewe nimekuweka kuwa mchunguzina mpimaji wa watu wangu,ili uchunguze na kuzijua njia zao.
28 Wote ni waasi wakaidi,ni watu wanaopitapita wakisengenya wengine,wagumu kama shaba nyeusi au chuma;wote hutenda kwa ufisadi.
29 Mifuo inafukuta kwa nguvu,risasi inayeyukia humohumo motoni;ni bure kuendelea kuwatakasa watu wangu,waovu hawawezi kuondolewa uchafu wao.
30 Wataitwa ‘Takataka za fedha’,maana mimi Mwenyezi-Mungu nimewakataa.”