9 Wenye hekima wenu wataaibishwa;watafadhaishwa na kunaswa.Wamelikataa neno la Mwenyezi-Mungu;je, ni hekima gani hiyo waliyo nayo?
10 Kwa hiyo, wake zao nitawapa watu wengine,mashamba yao nitawapa wengine.Maana, tangu mdogo hadi mkubwa,kila mmoja ana tamaa ya faida haramu.Tangu manabii hadi makuhani,kila mmoja anatenda kwa udanganyifu.
11 Wameliponya jeraha la watu wangu juujuu,wakisema, ‘Kuna amani, kuna amani’,kumbe hakuna amani yoyote!
12 Je, waliona aibu walipotenda machukizo hayo?La hasha! Hawakuona aibu hata kidogo.Hata hawajui kuona haya.Kwa hiyo, wataanguka pamoja na wale walioanguka;nitakapowaadhibu, wataangamia.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
13 “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema:Nilipotaka kukusanya chochote kutoka kwao,sikupata zabibu hata moja juu ya mzabibu,sikupata tini zozote juu ya mtini;hata majani yao yamekauka.Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.”
14 “Watu wanauliza: Kwa nini sisi tunakaa tu hapa?Kusanyikeni, tuingie katika miji yenye ngome,tukaangamie huko!Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametupangia tuangamie,ametupa maji yenye sumu tunywe,kwa kuwa tumemkosea yeye.
15 Tulitazamia kupata amani,lakini hakuna jema lililotokea.Tulitazamia wakati wa kuponywa,badala yake tukapata vitisho.