22 Nawe utajiuliza moyoni mwako,“Kwa nini mambo haya yamenipata?”Sawa! Kama vazi lako limepandishwa juu,nawe ukatendewa kwa ukatili mno,hayo ni matokeo ya makosa yako mengi mno.
23 Je, Mwethiopia aweza kubadili rangi yake,au chui madoadoa yake?Ikiwezekana, nanyi pia mnaweza kutenda mema,nyinyi mliozoea kutenda maovu!
24 Mwenyezi-Mungu atawatawanya kama makapiyanayopeperushwa na upepo kutoka jangwani.
25 Mwenyezi-Mungu asema:“Hayo ndiyo yatakayokupata,ndivyo nilivyoamua kukutenda mimi Mwenyezi-Mungu,kwa sababu umenisahau mimi,ukaamini miungu ya uongo.
26 Nitalipandisha vazi lako hadi kichwanina aibu yako yote itaonekana wazi.
27 Nimeyaona machukizo yako:Naam, uzinifu wako na uzembe wako,na uasherati wako wa kupindukia,juu ya milima na mashambani.Ole wako ee Yerusalemu!Mpaka lini utakaa bila kutakaswa?”