10 Msimlilie mtu aliyekufa,wala msiombolezee kifo chake.Bali mlilieni kwa uchungu yule aendaye mbali,kwa kuwa hatarudi tena kuiona nchi yake.
11 Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya Shalumu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, aliyetawala baada ya Yosia baba yake, na ambaye aliondoka mahali hapa: “Shalumu hatarudi tena mahali hapa,
12 bali atafia hukohuko walikomchukua utumwani. Kamwe hataiona tena nchi hii.
13 “Ole wako Yehoyakimuwewe unayejenga nyumba kwa dhulumana kuiwekea ghorofa bila kutumia haki.Unawaajiri watu wakutumikie burewala huwalipi mishahara yao.
14 Wewe wasema:‘Nitalijenga jumba kubwa,lenye vyumba vikubwa ghorofani.’Kisha huifanyia madirisha,ukafunika kuta zake kwa mbao za mierezi,na kuipaka rangi nyekundu!
15 Unadhani umekuwa mfalmekwa kushindana kujenga kwa mierezi?Baba yako alikula na kunywa,akatenda mambo ya haki na memandipo mambo yake yakamwendea vema.
16 Aliwapatia haki maskini na wahitaji,na mambo yake yakamwendea vema.Hii ndiyo maana ya kunijua mimi Mwenyezi-Mungu.