14 Wakamkabidhi Yeremia kwa Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, amchukue nyumbani kwake. Basi, Yeremia akaishi pamoja na wananchi wengine.
15 Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia wakati alipokuwa amefungwa katika ukumbi wa walinzi:
16 “Nenda ukamwambie hivi Ebedmeleki, Mwethiopia: Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama mimi nitatimiza mambo yale niliyotamka dhidi ya mji huo na sio mambo mema. Mambo hayo yatakamilika siku hiyo ukiona wewe mwenyewe.
17 Lakini siku hiyo mimi nitakuokoa wewe, wala hutatiwa mikononi mwa watu unaowaogopa.
18 Maana, kweli nitakuokoa na hutauawa vitani; utapata faida ya kuokoa maisha yako kwa sababu umeniamini mimi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”