21 Kwa kishindo cha kuanguka kwao, dunia itatetemeka; sauti ya kilio chao itasikika mpaka bahari ya Shamu.
22 Tazama, adui atapanda juu na kuruka kama tai na kutandaza mabawa yake juu ya Bosra. Siku hiyo moyo wa mashujaa wa Edomu utakumbwa na hofu kama ya mwanamke anayejifungua.”
23 Kuhusu Damasko:“Miji ya Hamathi na Arpadi, imejaa wasiwasikwa kufikiwa na habari mbaya;mioyo ya watu wake inayeyuka kwa hofu,imefadhaika kama bahari isiyoweza kutulia.
24 Watu wa Damasko wamekufa moyo;wamegeuka wapate kukimbia;hofu kubwa imewakumba,uchungu na huzuni vimewapata,kama mwanamke anayejifungua
25 Ajabu kuachwa kwa mji maarufu,mji uliokuwa umejaa furaha!
26 Basi vijana wake wataanguka viwanjani mwake,askari wake wote wataangamizwa siku hiyo.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.
27 Nitawasha moto katika kuta za Damasko,nao utateketeza ngome za mfalme Ben-hadadi.”