1 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nitachochea upepo wa kuangamiza dhidi ya Babuloni,dhidi ya wakazi wa Kaldayo.
2 Nitawapeleka wapepetaji Babuloni,nao watampepeta;watamaliza kila kitu katika nchi yakewatakapofika kuishambulia toka kila upandewakati wa maangamizi yake.”
3 Usiwape nafasi wapiga mshale wa Babuloni;usiwaache wavute upinde,wala kuvaa mavazi yao ya vita.Usiwahurumie vijana wake;liangamize kabisa jeshi lake.
4 Wataanguka na kuuawa katika nchi ya Wakaldayo,watajeruhiwa katika barabara zake.
5 Lakini Israeli na Yuda hawakuachwa na Mungu wao Mwenyezi-Mungu wa majeshi,ingawa nchi yao imejaa hatia mbele yake yeye Mtakatifu wa Israeli.
6 Kimbieni kutoka Babuloni,kila mtu na ayaokoe maisha yake!Msiangamizwe katika adhabu yake,maana huu ndio wakati wa Mungu wa kulipa kisasi,anaiadhibu Babuloni kama inavyostahili.