34 Mfalme Nebukadneza wa Babulonialiuharibu na kuuponda mji wa Yerusalemualiuacha kama chungu kitupu;aliumeza kama joka.Alijaza tumbo lake vitu vyake vizurivizuri,akautupilia mbali kama matapishi.
35 Watu wa Yerusalemu na waseme:“Babuloni na ulipizwe ukatili uleule,tuliotendwa sisi pamoja na jamaa zetu!Babuloni ipatilizwekwa umwagaji wa damu yetu.”
36 Kwa hiyo asema hivi Mwenyezi-Mungu:“Nitawatetea kuhusu kisa chenu,na kulipiza kisasi kwa ajili yenu.Nitaikausha bahari ya Babulonina kuvifanya visima vyake vikauke.
37 Babuloni itakuwa rundo la magofu,itakuwa makao ya mbweha,itakuwa kinyaa na kitu cha kuzomewa;hakuna mtu atakayekaa huko.
38 Wababuloni watanguruma pamoja kama simba;watakoroma kama wanasimba.
39 Wakiwa na uchu mkubwanitawaandalia karamu:Nitawalewesha mpaka wapepesuke;nao watalala usingizi wa daimana hawataamka tena.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
40 Nitawashusha chini kama kondoo wa kuchinjwa,kama vile kondoo dume na beberu.