12 Nyumba zao zitapewa watu wengine,kadhalika na mashamba yao na wake zao;maana nitaunyosha mkono wangu,kuwaadhibu wakazi wa nchi hii.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
13 Wote, tangu mdogo hadi mkubwa kabisa,kila mmoja anatamani kupata faida isiyo halali.Tangu manabii hadi makuhani,kila mmoja wao ni mdanganyifu.
14 Wameliponya jeraha la watu wangu juujuu,wanasema; ‘Amani, amani’,kumbe hakuna amani yoyote!
15 Je, waliona aibu walipofanya machukizo hayo?La! Hawakuona aibu hata kidogo.Hawakujua hata namna ya kuona aibu.Kwa hiyo wataanguka pamoja na wale waangukao;wakati nitakapowaadhibu,wataangamizwa kabisa.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
16 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Simameni katika njia panda, mtazame.Ulizeni mjue juu ya matukio ya zamani.Tafuteni mahali ilipo njia nzurimuifuate nanyi mtapumzisha nafsi zenu.Lakini wao wakasema:‘Hatutafuata njia hiyo.’
17 Kisha nikawawekea walinzi, nikawaambia:‘Sikilizeni ishara ya tarumbeta.’Lakini wao wakasema: ‘Hatutaisikiliza.’
18 “Kwa hiyo, sikilizeni enyi mataifa;enyi jumuiya ya watu jueni yatakayowapata.