19 Sikiliza ee dunia!Mimi nitawaletea maafa watu hawakulingana na nia zao mbaya.Maana hawakuyajali maneno yangu,na mafundisho yangu nayo wameyakataa.
20 Ya nini kuniletea ubani kutoka Sheba,na udi wa harufu nzuri kutoka nchi ya mbali?Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliki,wala tambiko zenu hazinipendezi.
21 Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Tazama, nitawawekea watu hawa vikwazoambavyo vitawakwaza na kuwaangusha chini.Akina baba na watoto wao wa kiume wataangamia,kadhalika na majirani na marafiki.”
22 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Tazameni, watu wanakuja toka nchi ya kaskazini;taifa kubwa linajitayarisha kutoka mbali duniani.
23 Wamezishika pinde zao na mikuki,watu wakatili wasio na huruma.Vishindo vyao ni kama ngurumo ya bahari.Wamepanda farasi,wamejipanga tayari kwa vita,dhidi yako ewe Siyoni!”
24 Waisraeli wanasema,“Tumesikia habari zao,mikono yetu imelegea;tumeshikwa na dhiki na uchungu,kama mwanamke anayejifungua.
25 Hatuwezi kwenda mashambani,wala kutembea barabarani;maadui wameshika silaha mikononi,vitisho vimejaa kila mahali.”