1 “Wakati huo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, mifupa ya wafalme wa Yuda, mifupa ya wakuu wao, mifupa ya makuhani, mifupa ya manabii na mifupa ya wakazi wote wa Yerusalemu itachimbuliwa makaburini mwao.
2 Itaachwa imetandazwa mbele ya jua na mwezi na sayari zote za mbinguni, vitu ambavyo walivipenda na kuvitumikia, wakavitaka shauri na kuviabudu. Mifupa hiyo haitakusanywa wala kuzikwa, bali itakuwa kama mavi juu ya ardhi.
3 Watu wote waliobaki wa jamaa hii mbovu, mahali popote pale nilipowatawanya, wataona heri kufa kuliko kuishi. Ndivyo nisemavyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
4 “Wewe Yeremia utawaambiakuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Mtu akianguka, je hainuki tena?Mtu akipotea, je, hairudii tena njia yake?
5 Mbona basi, watu hawa wameacha njia iliyo sawana kuendelea katika upotovu wao?Wanashikilia miungu yao ya uongo,na kukataa kunirudia mimi!
6 Mimi nilisikiliza kwa makini,lakini wao hawakusema ukweli wowote.Hakuna mtu anayetubu uovu wake,wala kujiuliza; ‘Nimefanya nini?’Kila mmoja wao anashika njia yake,kama farasi akimbiliavyo moja kwa moja vitani.
7 Hata korongo anajua wakati wa kuhama;njiwa, mbayuwayu na koikoi,hufuata majira yao ya kurudi.Lakini watu wangu hawa hawajui kitujuu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.