13 “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema:Nilipotaka kukusanya chochote kutoka kwao,sikupata zabibu hata moja juu ya mzabibu,sikupata tini zozote juu ya mtini;hata majani yao yamekauka.Hata nilichokuwa nimewapa kimetoweka.”
14 “Watu wanauliza: Kwa nini sisi tunakaa tu hapa?Kusanyikeni, tuingie katika miji yenye ngome,tukaangamie huko!Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametupangia tuangamie,ametupa maji yenye sumu tunywe,kwa kuwa tumemkosea yeye.
15 Tulitazamia kupata amani,lakini hakuna jema lililotokea.Tulitazamia wakati wa kuponywa,badala yake tukapata vitisho.
16 Sauti za farasi wao zinasikika,kwa mlio wa farasi wao wa vita,nchi nzima inatetemeka.Wanafika na kuiharibu nchi na vyote vilivyomo,kuangamiza mji pamoja na wote waishio humo.
17 “Basi nitawaleteeni nyoka;nyoka wenye sumu wasioweza kurogwa na walozi,nao watawauma nyinyi.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
18 Huzuni yangu haiwezi kutulizwa,moyo wangu wasononeka ndani yangu.
19 Sikiliza kilio cha watu wangu,kutoka kila upande katika nchi.“Je, Mwenyezi-Mungu hayuko Siyoni?Je, mfalme wake hayuko tena huko?”“Mbona wamenikasirisha kwa sanamu zao za miungu,na vinyago vyao vya miungu ya kigeni?”