3 Watu wote waliobaki wa jamaa hii mbovu, mahali popote pale nilipowatawanya, wataona heri kufa kuliko kuishi. Ndivyo nisemavyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
4 “Wewe Yeremia utawaambiakuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Mtu akianguka, je hainuki tena?Mtu akipotea, je, hairudii tena njia yake?
5 Mbona basi, watu hawa wameacha njia iliyo sawana kuendelea katika upotovu wao?Wanashikilia miungu yao ya uongo,na kukataa kunirudia mimi!
6 Mimi nilisikiliza kwa makini,lakini wao hawakusema ukweli wowote.Hakuna mtu anayetubu uovu wake,wala kujiuliza; ‘Nimefanya nini?’Kila mmoja wao anashika njia yake,kama farasi akimbiliavyo moja kwa moja vitani.
7 Hata korongo anajua wakati wa kuhama;njiwa, mbayuwayu na koikoi,hufuata majira yao ya kurudi.Lakini watu wangu hawa hawajui kitujuu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.
8 Mnawezaje kusema: ‘Sisi tuna hekima,sisi tunayo sheria ya Mwenyezi-Mungu,’hali waandishi wa sheria,wameipotosha sheria yangu?
9 Wenye hekima wenu wataaibishwa;watafadhaishwa na kunaswa.Wamelikataa neno la Mwenyezi-Mungu;je, ni hekima gani hiyo waliyo nayo?