22 Maiti za watu zimetapakaa kila mahalikama marundo ya mavi mashambani,kama masuke yaliyoachwa na mvunaji,wala hakuna atakayeyakusanya.’Ndivyo alivyoniambia Mwenyezi-Mungu niseme.”
23 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mwenye hekima asijivunie nguvu zake,wala tajiri asijivunie utajiri wake.
24 Anayetaka kujivuna na ajivunie jambo hili:Kwamba ananifahamukwamba anajua Mwenyezi-Mungu hutenda mema,hufanya mambo ya haki na uadilifu duniani.Watu wa namna hiyo ndio wanipendezao.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
25 Mwenyezi-Mungu asema: “Siku zaja ambapo nitawaadhibu wote waliotahiriwa mwilini tu:
26 Wamisri, Wayuda, Waedomu, Waamoni, Wamoabu na wakazi wote wa jangwani wanaonyoa denge. Maana watu hawa wote na Waisraeli wote hawakutahiriwa moyoni.”