1 Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu,ingawa nakulalamikia.Lakini ningependa kutoa hoja zangu mbele yako:Kwa nini waovu hufanikiwa katika mambo yao?Mbona wote wenye hila hustawi?
2 Unawaotesha nao wanaota;wanakua na kuzaa matunda.Wanakutaja kwa maneno yao,lakini mioyo yao iko mbali nawe.
3 Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu wanijua;wayathibiti maelekeo yangu kwako.Uwaokote hao kama kondoo wa kuchinjwa,watenge kwa ajili ya wakati wa kuuawa.
4 Mpaka lini nchi itaomboleza kwa ukame,na nyasi za mashamba yote kunyauka?Wanyama na ndege wanakufa kwa uovu wa wakazi wake;wanasema: “Mungu hataona mwisho wetu.”
5 Mwenyezi-Mungu asema,“Ikiwa umeshindana na waendao kwa miguu ukachoka,utawezaje kushindana na farasi?Kama unaanguka katika nchi isiyo na vizuizi,utafanyaje katika msitu wa Yordani?
6 Hata ndugu zako, jamaa yako mwenyewe,nao pia wamekutendea mambo ya hila;wanakukemea waziwazi.Usiwaamini hata kidogo,japo wanakuambia maneno mazuri.”
7 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nimeiacha nyumba yangu;nimeitupa mali yangu mimi mwenyewe.Israeli, mpenzi wangu wa moyo,nimemtia mikononi mwa maadui zake.