5 Mwenyezi-Mungu asema,“Ikiwa umeshindana na waendao kwa miguu ukachoka,utawezaje kushindana na farasi?Kama unaanguka katika nchi isiyo na vizuizi,utafanyaje katika msitu wa Yordani?
6 Hata ndugu zako, jamaa yako mwenyewe,nao pia wamekutendea mambo ya hila;wanakukemea waziwazi.Usiwaamini hata kidogo,japo wanakuambia maneno mazuri.”
7 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nimeiacha nyumba yangu;nimeitupa mali yangu mimi mwenyewe.Israeli, mpenzi wangu wa moyo,nimemtia mikononi mwa maadui zake.
8 Wateule wangu wamenigeuka,wamekuwa kama simba porini,wameningurumia mimi;ndiyo maana nawachukia.
9 Wateule wangu wamekuwa ndege mzuriwanaoshambuliwa na kozi pande zote.Nenda ukawakusanye wanyama wote wakaliwaje kushiriki katika karamu.
10 Wachungaji wengi wameharibu shamba langu la mizabibu,wamelikanyagakanyaga chini lililo mali yangu;shamba langu zuri wamelifanya jangwa.
11 Wamelifanya kuwa tupu;katika ukiwa wake lanililia.Nchi yote imekuwa jangwa,wala hakuna mtu anayejali.