14 Nitawagonganisha wao kwa wao kina baba na watoto. Sitawahurumia, sitawaachia wala sitawarehemu, bali nitawaangamiza.”
15 Enyi Waisraeli, sikilizeni kwa makini,msiwe na majivuno maana Mwenyezi-Mungu anasema nanyi.
16 Mtukuzeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,kabla hajawaletea giza,nanyi mkajikwaa miguu kwenye milima ya giza.Nyinyi mnatazamia mwanga,lakini anaugeuza kuwa utusitusina kuufanya kuwa giza nene.
17 Lakini kama msiponisikiliza,moyo wangu utalia machozi faraghani,kwa sababu ya kiburi chenu.Nitalia kwa uchungu na kububujika machozi,kwa kuwa watu wa Mwenyezi-Mungu wametekwa.
18 Mwambie mfalme na mama yake hivi:“Shukeni kwenye viti vyenu vya enzi,maana taji zenu nzuri zimeanguka vichwani mwenu.
19 Miji ya Negebu imezingirwa;hakuna awezaye kufungua malango yake.Watu wa Yuda wamechukuliwa mateka,wote kabisa wamepelekwa utumwani.”
20 Inua macho yako, ee Yerusalemu!Tazama! Madui zako waja kutoka kaskazini.Kundi ulilokabidhiwa liko wapi?Kundi lako zuri li wapi?