2 “Nenda ukawatangazie waziwazi wakazi wote wa Yerusalemu kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Naukumbuka uaminifu wako ulipokuwa kijana,jinsi ulivyonipenda kama mchumba wako,ulivyonifuata jangwanikwenye nchi ambayo haikupandwa kitu.
3 Israeli, wewe ulikuwa mtakatifu kwangu,ulikuwa matunda ya kwanza ya mavuno yangu.Wote waliokudhuru walikuwa na hatia,wakapatwa na maafa.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
4 Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu, enyi wazawa wa Yakobo. Sikilizeni enyi jamaa zote za wazawa wa Israeli.
5 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Wazee wenu waliona kosa gani kwanguhata wakanigeuka na kuniacha,wakakimbilia miungu duni,hata nao wakawa watu duni?
6 Hawakujiuliza:‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu aliyetutoa nchini Misri,aliyetuongoza nyikanikatika nchi ya jangwa na makorongo,nchi kame na yenye giza nene,nchi isiyopitiwa na mtu yeyote,wala kukaliwa na binadamu?’
7 Niliwaleta katika nchi yenye rutuba,muyafurahie mazao yake na mema yake mengine.Lakini mlipofika tu mliichafua nchi yangu,mkaifanya chukizo nchi niliyowapa iwe yenu.
8 Nao makuhani hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu?’Wataalamu wa sheria hawakunijua,viongozi wa watu waliniasi;manabii nao walitabiri kwa jina la Baalina kuabudu sanamu zisizo na faida yoyote.”