5 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Wazee wenu waliona kosa gani kwanguhata wakanigeuka na kuniacha,wakakimbilia miungu duni,hata nao wakawa watu duni?
6 Hawakujiuliza:‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu aliyetutoa nchini Misri,aliyetuongoza nyikanikatika nchi ya jangwa na makorongo,nchi kame na yenye giza nene,nchi isiyopitiwa na mtu yeyote,wala kukaliwa na binadamu?’
7 Niliwaleta katika nchi yenye rutuba,muyafurahie mazao yake na mema yake mengine.Lakini mlipofika tu mliichafua nchi yangu,mkaifanya chukizo nchi niliyowapa iwe yenu.
8 Nao makuhani hawakujiuliza: ‘Yuko wapi Mwenyezi-Mungu?’Wataalamu wa sheria hawakunijua,viongozi wa watu waliniasi;manabii nao walitabiri kwa jina la Baalina kuabudu sanamu zisizo na faida yoyote.”
9 Mwenyezi-Mungu asema,“Kwa hiyo, mimi nitawalaumu nyinyi,na nitawalaumu wazawa wenu.
10 Haya, vukeni bahari hadi Kupro mkaone,au tumeni watu huko Kedari wakachunguze,kama jambo kama hili limewahi kutokea:
11 Kwamba kuna taifa lililowahi kubadilisha miungu yakeingawa miungu hiyo si miungu!Lakini watu wangu wameniacha mimi, utukufu wao,wakafuata miungu isiyofaa kitu.