4 Kama mkishika neno hili nililowaambia basi, wafalme wanaokikalia kiti cha enzi cha Daudi wataendelea kuingia kwa kupitia malango ya ikulu hii. Watapita pamoja na watumishi wao na watu wao, wakiwa wamepanda farasi na magari ya farasi.
5 Lakini kama hamtatii maneno haya, mimi Mwenyezi-Mungu naapa kwa nafsi yangu kwamba mahali hapa patakuwa magofu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
6 Mwenyezi-Mungu asema hivi kuhusu ikulu ya mfalme wa Yuda:“Ingawa waonekana kuwa mzuri kama nchi ya Gileadikama kilele cha Lebanoni,Lakini naapa kuwa nitakufanya uwe jangwa,uwe mji usiokaliwa na watu.
7 Nitawatayarisha waangamizi dhidi yako,kila mmoja na silaha yake mkononi.Wataikata mierezi yako mizuri,na kuitumbukiza motoni.
8 “Kisha watu wengi wa mataifa watapita karibu na mji huu, na kila mmoja atamwuliza mwenzake: ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu ameutenda hivi mji huu mkubwa?’
9 Wenzao watawajibu, ‘Ni kwa sababu waliliacha agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, wakaiabudu miungu mingine na kuitumikia.’”
10 Msimlilie mtu aliyekufa,wala msiombolezee kifo chake.Bali mlilieni kwa uchungu yule aendaye mbali,kwa kuwa hatarudi tena kuiona nchi yake.