11 Mwenyezi-Mungu amezichochea roho za wafalme wa Media, kwa maana amenuia kuiangamiza Babuloni. Naam, hicho ndicho kisasi cha Mwenyezi-Mungu; analipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake.Noeni mishale yenu!Chukueni ngao!
12 Twekeni bendera ya vitakushambulia kuta za Babuloni.Imarisheni ulinzi;wekeni walinzi;tayarisheni mashambulizi.Mwenyezi-Mungu amepanga na kutekelezamambo aliyosema juu ya wakazi wa Babuloni.
13 Nchi hiyo imejaa mito na hazina tele,lakini mwisho wake umefika,uzi wa uhai wake umekatwa.
14 Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa kwa nafsi yake:“Hakika nitakujaza majeshi mengi kama nzige,nayo yatapiga vigelegele vya ushindi juu yako”
15 Mwenyezi-Mungu ndiye aliyeumba dunia kwa nguvu yake,aliyeuimarisha ulimwengu kwa hekima yake,na kwa maarifa yake akazitandaza mbingu.
16 Anapotoa sauti yake maji hutitima mbinguni,hufanya ukungu upande kutoka mipaka ya dunia.Hufanya umeme umulike wakati wa mvuahuvumisha upepo kutoka ghala zake.
17 Kila mtu ni mpumbavu bila maarifa,kila mhunzi anaaibishwa na vinyago vyake;maana sanamu zake ni udanganyifu mtupu,wala hazina pumzi ndani yake.