4 “Wewe Yeremia utawaambiakuwa mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Mtu akianguka, je hainuki tena?Mtu akipotea, je, hairudii tena njia yake?
5 Mbona basi, watu hawa wameacha njia iliyo sawana kuendelea katika upotovu wao?Wanashikilia miungu yao ya uongo,na kukataa kunirudia mimi!
6 Mimi nilisikiliza kwa makini,lakini wao hawakusema ukweli wowote.Hakuna mtu anayetubu uovu wake,wala kujiuliza; ‘Nimefanya nini?’Kila mmoja wao anashika njia yake,kama farasi akimbiliavyo moja kwa moja vitani.
7 Hata korongo anajua wakati wa kuhama;njiwa, mbayuwayu na koikoi,hufuata majira yao ya kurudi.Lakini watu wangu hawa hawajui kitujuu ya amri zangu mimi Mwenyezi-Mungu.
8 Mnawezaje kusema: ‘Sisi tuna hekima,sisi tunayo sheria ya Mwenyezi-Mungu,’hali waandishi wa sheria,wameipotosha sheria yangu?
9 Wenye hekima wenu wataaibishwa;watafadhaishwa na kunaswa.Wamelikataa neno la Mwenyezi-Mungu;je, ni hekima gani hiyo waliyo nayo?
10 Kwa hiyo, wake zao nitawapa watu wengine,mashamba yao nitawapa wengine.Maana, tangu mdogo hadi mkubwa,kila mmoja ana tamaa ya faida haramu.Tangu manabii hadi makuhani,kila mmoja anatenda kwa udanganyifu.